Yahya Douri mkuu wa masuala ya muongozo wa Kiislamu katika wizara hiyo amesema aghalabu ya waliosilimu mwaka huu ni raia wa Ufaransa wanaofanya kazi nchini Algeria huku idadi ya Wachina wanaosilimu ikiongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
Amesema idadi ya wanaosilimu ni kubwa zaidi ya hii kwani takwimu zilizotajwa ni za wale wanaotangaza rasmi kukubali Uislamu.
Idadi kubwa ya watu waliosilimu wako katika miji ya Algeiers na Tizi-Ouzou. 'Waliosilimu wamefanya hivyo kwa hiari yao baada ya kusoma kwa kina mafundisho ya Uislamu', amesema afisa huyo. Aidha kufunga ndoa na raia wa Algeria pia kumetajwa kuchangia kwa kiasi kubwa idadi ya wanaosilimu ambao huvutiwa na mfumo wa kijamii wa Kiislamu.
831344