IQNA

Kikao cha 'Tarjumi na Balagha ya Qur'ani Tukufu' kufanyika Morocco

23:56 - July 25, 2011
Habari ID: 2159810
Kikao cha Tatu cha Kimataifa cha Qur'ani Tukufu chini ya anuani ya "Tarjumi na Balagha ya Qur'ani Tukufu' kitafanyika Morocco tarehe 22-23 Mei mwaka 2012.
Kikao hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Dar Al-Hadith Al-Hassania ya Rabat kwa ushirikiano na Kituo cha Tafsiri ya Qur'ani nchini humo. Wasomi na wataalamu kutoka nchi mbalimbali duniani wanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo.
Kati ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na 'Balagha ya Qur'ani na Nadharia ya Tarjumi', 'Kuhifadhi Balagha Katika Tarjumi', 'Kutarjumi Balagha ya Qur'ani', 'Tarjumi ya Lugha Asili na Lugha Kusudiwa na Changamoto Zake' na 'Changamoto za Balagha ya Qur'ani' kati ya mada zinginezo.
831274
captcha