Sheikh Ahmad Tayyib ambaye jana alifanya mazungumzo na ujumbe wa maulamaa wa Kishia na Kisuni kutoka Lebanon amesisitiza juu ya udharura wa kulindwa umoja na mshikamano kati ya Shia na Suni.
Amesema wafuasi wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu wanapaswa kupiga hatua zaidi mbele katika njia ya ushindi wa Uislamu kwa kuimarisha maelewano, umoja na mshikamano wao.
Sheikh wa al Azhar amesisitiza kuwa umoja wa Kiislamu unawezekana kupitia njia ya kuheshimiana na kila upande kuukubali mwingine. Amesema kuwa kuwavunjia heshima Ahlulbait (as) na masahaba wa Mtume ni mstari mwekundu ambao haupaswi kuvukwa na yeyote na amewataka maulamaa wa Kishia na Kisuni kutoa fatuwa zinazoharamisha kuwavunjia heshima watukufu hao. 832005