IQNA

Chuo cha Al Azhar chalaani ugaidi Norway

13:22 - July 27, 2011
Habari ID: 2160775
Chuo Kikuu cha Al Azhar kimelaani hujuma za kigaini Norway na kusema hujuma hizo ni ishara ya hatari itokanayo na mirengo ya kulia yenye misimamo mikali katika nchi za Magharibi.
Taarifa ya Al Azhar imeelezea matumaini kuwa hujuma hiyo itaimarisha azma ya Norway ya kueneza amani na usalama kwa watu wote wa Mashariki na Magharibi.
Mashambulizi ya Norway yaliyopelekea makumi ya watu kuuawa yanaendelea kulaani duniani.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) pia imelaani hujuma za kigaidi nchini Norway.
Katibu Mkuu wa OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu amesema, ‘Kufuatia hujuma za kigaidi nchini Norway, tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia za wahanga, serikali na wananchi wa nchi hii”.
Katibu Mkuu wa OIC emetoa wito wa kuendelezwa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na ugaidi.
832449
captcha