IQNA

Demokrasia haiwezekani bila Uislamu

13:16 - July 27, 2011
Habari ID: 2160787
Mwanazuoni wa Kiislamu nchini Iran amesema mfumo wa demokrasia na jamhuri hauwezi kufanikiwa pasina kuwepo Uislamu.
Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Qaim Maqami ameongeza kuwa Uislamu ndio njia pekee ya kuzuia udikteta.
‘Baadhi ya wanamapinduzi wanadai kuwa mwamko katika ulimwengu wa Kiislamu hauna uhusiano na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika hali ambayo Mapinduzi ya Kiislamu yamekita mizizi katika nchi za Kiislamu’.
Amesema nukta zinazozingatiwa katika Mapinduzi ya Kiislamu ni kushirikishwa wananchi kikamilifu katika uendeshaji wa nchi. ‘Hii ni demokrasia na jamhuri. Nukta nyingine ni kufuatwa mafunzo ya Kiislamu ili kuhakikisha kuwa jamhuri inadumu’. Amesema wananchi wa eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika wanataka nchi zao ziendeshwe kwa msingi wa Uislamu na ndio sababu maandamano mengi yanafanyika baada ya sala ya Ijumaa.
Mwanazuoni huyo amesema mifarakano ya kimadhehebu haina nafasi katika maeneo hayo. Ameonya kuhusu njama za Marekani za kutaka kuvuruga mwamko wa Kiislamu.
832247
captcha