IQNA

Waziri Mkuu wa Norway atembelea Mskiti wa Oslo

18:58 - July 30, 2011
Habari ID: 2162179
Waziri Mkuu wa Norway Jens Stoltenberg ametembelea Msikiti wa Oslo ikiwa ni katika kuwajulia hali Waislamu baada ya mashambulizi ya kigaidi ya wiki iliyopita ambayo yalisababisha vifo vya makumi ya watu nchini humo.
Jens Stoltenberg alishiriki katika majlisi maalumu ya Waislamu ya kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Mkristo mwenye misimamo mikali na chuki dhidi ya Wialamu juma lililopita.
Waziri Mkuu wa Norway alifuatana na Askofu wa mji wa Oslo katika ziara hiyo na kushiriki katika majlisi ya dua ya Waislamu wa mji huo.
Jens Stoltenberg alisema katika hotuba fupi msikitini hapo kwamba Oslo inaheshimu amani, urafiki na sera za kupambana na chuki na inasisitiza juu ya umoja wa Norway.
Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu wa Norway alisema kuwa matukio ya siku chache zilizopita nchini humo ni mashambulizi ya kigaidi. Amesema Waislamu wa nchi hiyo wataendelea kuwa bega kwa bega na raia wenzao katika masaibu hayo. 833820


captcha