IQNA

Kitengo cha Kimataifa cha maonyesho ya Qur’ani Tehran

23:31 - July 31, 2011
Habari ID: 2162809
Mkurugenzi wa kitengo cha kimataifa katika Maonyesho ya 19 ya Qur’ani ya Tehran amesema kitengo hicho kinaonyesha mafanikio ya shughuli za Qur’ani duniani.
Akizungumza na IQNA, Ali Reza Esmaili amesema malengo matatu muhimu ya kitengo cha kimataifa ni kutoa fursa kwa wasomi na watafiti wa Qur’ani kubadilishana mawazo na vilevile kuanzisha mawasiliano baina taasisi mbalimbali za Qur’ani duniani.
Ameongeza kuwa watarjumi kadhaa wa Qur’ani kutoka nchi kama vile Pakistan, Ufilipino na Kenya wanashiriki katika maonyesho ya mwaka huu mjini Tehran.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tehran yalianza Julai 28 na yataendelea hadi tarehe 25 ya mwezi wa Ramadhani.
Kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu ni ‘Qur’ani Kitabu cha Mwamko’.
834436
captcha