Fedha hizo zimewekwa katika akaunti nambari 99999 ya Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye Benki ya Melli nchini Iran.
Eneo la Pembe ya Afrika hususa nchi ya Somalia limekumbwa na baa kubwa la njaa lililosababishwa na ukame na uhaba wa mvua. Jumuiya za kimataifa zinasema kuwa watu milioni 10 wanatishiwa na hatari ya njaa na kwamba kuna udharura wa kutumwa misaada ya kibinadamu kwa watu wa eneo hilo haraka iwezekanavyo.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tayari imetuma shehena kadhaa za misaada ya kibinadamu kwa Waislamu waliokumbwa na maafa ya njaa nchini Somalia. 834771