Ahmad Davutoglu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akizungumza na waandishi habari wa Uturuku amesema hali ya watu wa nchi kadhaa za Afrika ni ya kusikitisha. Ametaka OIC iitishe kikao kujadili njia za kutuma misaada nchini katika Pembe ya Afrika.
Davutoglu amesema amezungumza na Katibu Mkuu wa OIC Profesa Ekmaeleddin Ihsanoglu na kumtaka aitishe kikao cha dharura kujadili kadhia ya njaa Afrika. Amesema Uturuki inatuma ujumbe Ethiopa, Kenya na nchi kadhaa za Afrika kwa lengo la kuwasaidia wenye njaa. 837757