Waandamanaji wametoa nara ya 'Ijumaa ya Amani Hadi Ushindi' na wametaka harakati ziendelee hadi mapinduzi yafikie malengo yake.
Ali Abdalllah Saleh, dikteta wa Yemen ambaye bado yuko nchini Saudi Arabia alikokwenda kupata matibabu ametoa wito wa kuweko mazungumzo baina ya serikali yake na wapinzani. Rais wa Yemen ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 33 amesema kwamba, kuna haja ya kuweko mazungumzo na wapinzani na kutaka kutumiwa fursa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo. Dikteta wa Yemen ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na wapinzani bila ya kutangaza masharti.
Wakati huo huo, maandamano yanayompinga kiongozi huyo wa Yemen yameendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo. Aidha wananchi wa Yemen wameendelea kuzitaka tawala za Marekani na Saudi Arabia kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi yao.
837748