Khalid al Qaddumi ameiambia IQNA kwamba matunda muhimu zaidi ya harakati ya mageuzi ya wananchi wa kanda hii ni kurejesha utambulisho wa Kiislamu. Ameongeza kuwa utambulisho wa Kiislamu unawakusanya pamoja Waislamu kote duniani chini ya bendera ya umma wa Kiislamu.
Amesema matunda mengine ya harakati ya sasa ya wananchi katika nchi za Kiarabu ni kuwafanya Waislamu kote duniani wazingatie na kutilia maanani suala la Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni wa Israel. Al Qaddumi amesema, leo hii kadhia ya Palestina imekuwa kadhia ya umma mzima wa Kiislamu na Waislamu wanatambua kuwa wanawajibika kuilinda na kuitetea Palestina.
Mwakilishi wa Hamas nchini Iran amesema wimbi la mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika limehama kutoka nchi moja hadi nyingine na kuenea kati ya Waislami wote. 840656