Kikao cha kwanza cha kesi ya dikteta wa Misri kilifanyika tarehe 3 Agosti ambapo Mubarak alisomewa mashtaka yake. Miongoni mwa mashtaka hayo ni kutoa amri ya kuua wananchi waliokuwa wakipigania demokrasia.
Kabla ya kuondolewa madarakani, utawala wa Mubarak ulijaribu kuzima mapinduzi ya wananchi wa Misri kwa kutoa amri ya kuuawa kwa umati wananchi aliokuwa wakiandamana mitaani.
Tuhuma nyingine zinazomkabili Firauni wa Misri ni ufisadi, kutumia vibara madaraka yake na kuuza gesi ya taifa la Misri kwa utawala haramu wa Israel kwa bei ya kutupa.
Hussein Salim, rafiki na muitifaki wa karibu wa Hosni Mubarak ambaye ametumia mkataba wa kuiuzua gesi Israel kwa ajili ya kujitajiri, ni miongoni mwa watu wanaohukumiwa pamoja na dikteta huyo wa zamani wa Misri. Wengine ni wanawe wawili Gamal na Alaa, waziri wa zamani wa mambo ya ndani Habib al Adili na wasaidizi wake sita.
Katika kikao cha kwanza cha kesi hii, Mubarak na jamaa zake walikana tuhuma zote zinazowakabili.
Kikao cha kwanza cha kesi hii kiligubikwa pia na machafuko yaliyohusisha askari usalama na wafuasi wachache wa Mubarak waliokuwa nje ya mahakama ya Cairo. Kundi hili dogo pia limeapa kwamba litakusanyika tena leo mbele ya mahakama ya Cairo kuonyesha upinzani wake dhidi ya kesi inayomkabili dikteta wa Misri.
Ripoti za kuaminika zinasema kuwa, Marekani na Saudi Arabia zimetenga bajeti maalumu ya fedha zinazotolewa kama hongo kwa vyombo vya habari na wanasheria ili kuzuia au kupunguza anga inayopinga utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Misri ambayo ilitanda na kueneza zaidi baada ya mapinduzi ya wananchi mapema mwaka huu.
Kwa sasa Washington na Riyadh zinafanya jitihada kubwa za kuhakikisha kwamba mahakama ya kesi ya Mubarak inajiepusha kufichua siri kubwa na za kutisha zinazohusu washirika wa dikteta huyo na uhusiano wake mpana zaidi na utawala ghasibu wa Israel. Kwa msingi huo juhudi zinafanyika ili kesi hiyo itilie maanani zaidi kadhia ya uuzaji wa gesi ya Misri kwa Israel badala ya masuala mengine tata na muhimu zaidi.
Kikao cha leo cha kesi ya Mubarak kitahusu faili la mauaji na ukandamiza uliofanywa na utawala wa dikteta huyo dhidi ya wanamapinduzi wa Misri. Iwapo dikteta huyo atapatikana na hatia ya kuamuru mauaji dhidi ya raia, atahukumiwa kifo.
Weledi wa mambo wanasema kuwa kesi ya dikteta huyo ni kengele ya hatari kwa viongozi wengine wa nchi za Kiarabu na hata Afrika wanaolewa madaraka na kusahau kwamba itakuja siku ya mahesabu na kusimamishwa kizimbani.843582