IQNA

Maandamano ya kutetea Quds kufanyika Uingereza

17:15 - August 16, 2011
Habari ID: 2171696
Maandamano ya kutetea Wananchi wa Palestina pamoja na Quds Tukufu yamepangwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 21 Agosti huko London mji mkuu wa Uingereza.
Kwa mujibu wa tovuti ya aimislam, maandamano hayo ambayo yameandaliwa na Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza, yamepangwa kufanyika kuanzia saa 8 hadi saa 12 za jioni kwa wakati wa Uingereza mbele ya jengo la studio za Idhaa ya BBC.
Mashirika na taasisi mbalimbali za Uingereza, ikiwemo Jumuiya ya Kituo cha Kiislamu cha Uingereza, Jamii ya Marafiki wa Msikiti wa al-Aqsa, Jamii ya Kiislamu ya Ulaya, Jumuiya ya Wanachuo wa Kiislamu, Jamii ya Mayahudi Wanaopinga Utawala wa Kizayuni, Muungano wa Kiislamu wa Uingereza, Baraza la Kiislamu la Uingereza na Taasisi ya Mfungamano na Palestina ya Scotland zimetangaza kuwa zitashiriki katika maandamano hayo makubwa.
Kwa kujibu wa habari za kuaminika, maandamano hayo yatatangaza wazi uungaji mkono wake kwa haki za wananchi madhlumu wa Palestina na kufanya juhudi za kusimamisha ukandamizaji na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina. 843586
captcha