Kwa mujibu wa Abdulrauf al Shaib Msemaji wa Muungano wa 14 Februari wa Bahrain, Wabahraini sasa hawataki mabadiliko ya kisiasa bali takwa lao la pekee ni kuondoka Aal Khalifa madarakani na wananchi wapewa haki ya kuainisha hatima ya nchi yao. Amesema utawala wa Aal Khalifa hauna chaguo jingine isipokuwa kuondoka madarakani.
Mwanaharakati huyo aliye uhamishoni huko London Uingereza amesema utawala wa Aal Khalifa umeingiza vikosi vya kigeni nchini Bahrain kwa lengo la kuwakandamiza waandamanaji. Amesema kitendo hicho cha watawala wa Bahrain kimepelekea wananchi kutokuwa na imani nao kabisa na kwa hivyo wanapaswa kusikiliza matakwa ya wananchi na kuondoka madarakani.
Tokea mwezi Februari mwaka huu, utawala wa kifalme wa Aal-Khalifa unakabiliwa na harakati za mwamko wa wananchi wa Bahrain wanaotaka kuung'oa utawala wa kidikteta wa Al Khalifa ambao umetawala nchi hiyo kwa miaka 40 sasa.
846119