Huku akiashiria athari kubwa ya matukio yanayoendelea katika nchi za Kiarabu kwa suala la Palestina, mwanachama mmoja wa ngazi za juu katika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema kwamba maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Quds, ambayo hufanyika kila Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, yatakuwa tofauti kabisa na ya miaka iliyopita na kwamba utawala haramu wa Israel una wasiwasi mkubwa kuhusiana na jambo hilo.
Akizungumza hapo jana Jumatatu na televisheni ya al-Alaam, Khalil Abu Leila amesema kwamba kwa kutilia maanani maandamano na mikusanyiko mikubwa ambayo ilifanyika siku ya Nakama, ambayo ni siku ya kuanza kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na kuasisiwa rasmi utawala haramu wa Israel katika ardhi hizo, maandamano ya mwaka huu ya Siku ya Kimatafa ya Quds yatakuwa makubwa zaidi kuliko miaka mingine yote. Abu Leila amesema kuwa suala la Palestina ni suala la ulimwengu mzima wa Kiislamu na sio Walestina tu na kwa msingi huo kuwataka Waislamu wote duniani walichukulie suala hilo kuwa miongoni mwa majukumu yao makuu. 848098