Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran imesema kwamba, katika siku ya leo iliyotangazwa kama siku maalumu ya kuonyesha mshikamano wa Wairani kwa wananchi wa Somalia' wananchi wenye upendo wa Iran wamejitokeza kwa wingi katika vituo na sehemu za kukusanyia misaada za jumuiya hiyo na kutoa misaada ya fedha na isiyo ya fedha kwa ajili ya wananchi wa Somalia.
Wananchi wa Iran ambao siku zote wamekuwa pamoja na mataifa mengine duniani katika tabu na matatizo, leo pia wameonyesha moyo wao wa kujitolea kwa kuwasaidia wananchi wa Somalia wanaokabiliwa na njaa.
Vituo vya Jumuiya ya Misaada ya Iran ya Hilali Nyekundu pia vitakuwa wazi nchi zima katika Siku ya Kimataifa ya Qud na siku ya Idul Fitri kwa ajili ya kukusanya misaada ya fedha na isiyo ya fedha kwa ajili ya wananchi wa Iran.
848288