IQNA

Kikao cha kimataifa cha dini za mbinguni kufanyika Canada

14:57 - August 24, 2011
Habari ID: 2175976
Kikao cha kimataifa kuhusu dini za mbinguni kimepangwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Montreal Canada tarehe 7 Septemba.
Kikao hicho kinadhaminiwa na Vyuo Vikuu vya Montreal na McGill. Kikao hicho ambacho kitafanyika chini ya anwani ya 'Dini Baada ya Tukio la Septemba 11' kitafunguliwa kwa hotuba ya Dalai Lama, Kiongozi wa Mabudha wa Tibet.
Tariq Ramadhan, mtaalamu wa masuala ya Kiislamu anayeishi nchini Uswisi na mhadhiri wa Chuo cha Oxford na Deepak Jubra, tabibu wa Kihindi anayeishi nchini Marekani ambaye pia ameandika kitabu kuhusiana na tiba ya kiroho, ni miongoni mwa shakhsia, wasomi na wawakilishi wa dini mbalimbali ambao wamealikwa kushiriki mkutano huo wa kimataifa, ambao lengo lake ni kuimarisha amani duniani kupitia mafundisho ya kidini na mazungumzo ya maelewano kati jamii na mataifa mbalimbali.
Kikao hicho kitajadili maudhui tofauti zikiwemo za dini na haki za binadamu, uhubiri na uhuru wa dini, dini na umaanawi, dini na sayansi, dini na elimu ya tiba, dini na wanawake na pia dini na vyombo vya habari.
Kituo cha Makanisa ya Canada, Kituo cha Amani cha Canada, Taasisi ya Dalai Lama, Baraza la Kimataifa la Uhusiano la Montreal, Taasisi ya Familia ya Canada na mashirika mengine ya Kikristo na Kiislamu yanashirikiana katika kufanikisha kikao hicho. 848510
captcha