IQNA

Wapakistan kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds

15:24 - August 24, 2011
Habari ID: 2176275
Taasisi mbalimbali za kidini nchini Pakistan zimetangaza kuwa zitaandaa maandamano makubwa katika Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo huadhimishwa katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Jumuiya ya Imamiya ya Wanafunzi wa Pakistan ISO imesema itashiriki katika Siku ya Quds kwa lengo la kudhihirisha mfungamano wake na watu wa Palestina na kulaani utawala haramu wa Israel unaiokalia Quds Tukufu kwa mabavu.
Aidha Muungano wa Kimataifa wa Maulamaa na Mashekhe wa Pakistan WUUMC umetangaza kuwa Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani (Jumuatul Widaa) itaadhimishwa kama Siku ya Quds kwa lengo la kuwapa himaya Wapalestina wanaodhulumiwa katika minyororo ya Wazayuni maghasibu.
Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yatafanyika katika miji mbalimbali ya Pakistan kama vile Lahore, Karachi, Peshawar, Quetta, Mirpur, Multan, Faisalabad na Hyderabad.
848917
captcha