IQNA

Rais Ahmadinejad:

Iran inatumia uwezo wake wa kijeshi kukabiliana na dhulma

15:30 - August 24, 2011
Habari ID: 2176280
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amesema kamwe taifa la Iran halitatumia uwezo mkubwa wa jeshi lake dhidi ya binadamu wasiokuwa na hatia au kwa ajili ya kunyakua au kuzikalia kwa mabavu ardhi za nchi zingine.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo wakati wa kuzindua silaha mpya za Jeshi la Ulinzi la Iran likiwemo kombora la majini la Qadir linaloweza kupiga meli na manowari za kivita kutokea umbali ya kilomita mia mbili na mfumo wa kurushia makombora ya majini ya Topidi.
Rais Ahmadinejad amesema kuwa, uwezo mkubwa wa jeshi la Iran ni kwa ajili ya kuwalinda wananchi wake, kuzima njama za maadui na kuzuia dhulma ya aina yoyote dhidi ya taifa hili. Rais wa Iran ameongeza kuwa, jeshi la Iran liko tayari kuzima shambulizi lolote la adui na kuwa halitairuhusu nchi yoyote ile kulidhalilisha taifa hili la Kiislamu.
Wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ahmad Vahidi alisema taifa la Iran linaelekea kuwa miongoni mwa nchi tano zenye nguvu kubwa zaidi ya kijeshi duniani. Mafanikio haya ya Iran yamepatikana licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kislamu.
848574
captcha