Maandamano makubwa ya Waislamu kote duniani katika siku hiyo ni pigo kali dhidi ya ubeberu wa kimataifa. Maandamano hayo pia yanawahimiza Waislamu kote dunia kuwa macho na kuamka zaidi.
Imepita miaka 32 sasa tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yaliyoongozwa na Imam Ruhullah Khomeini ambaye aliasisi serikali ya kisasa na kuwarejesha Wairani katika utamaduni wa Kiislamu. Mapinduzi hayo yalipandikiza mbegu ya mwamko wa Kiislamu katika nyoyo za mataifa mbalimbali kwa kadiri kwamba wataalamu wa mambo wanaamini kwamba, mwamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa kwa sasa katika eneo la kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati ni athari na matokeo ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
Sambamba na hayo mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Ruhullah Khomeini alilipa kipaumbele suala la Palestina na Quds Tukufu na kuitangaza Ijuma ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kuwa ni siku ya kuonyesha mfungamano na wananchi wanaokandamizwa wa Palestina. Hatua hiyo ya Imam imewafanya watu wa mataifa, dini na kaumu tofauti kudhihirisha chuki na hasira yao dhidi ya mauaji yanayofanywa kila siku dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Palesina.
Kwa kuzingatia yote hayo tunaweza kusema kuwa maandamano ya Waislamu kote duniani katika Siku ya Kimataifa ya Quds yanatoa kipigo kikali dhidi ya mabebebru wa kimataifa hususan katika mwaka huu ambapo kunashuhudiwa harakati kubwa ya mwamko wa wananchi katika nchi mbalimbali za Kiislamu.
Maandamano ya Ijumaa ijayo ya Siku ya Kimataifa ya Quds pia yanazihimiza jumuiya za kimataifa hususan Umoja wa Mataifa na kuzitaka zitekeleza majukumu yao kuhusu wananchi wanaokandamizwa na Palestina. 849117