Siku ya Kimataifa ya Quds huwakumbusha Waislamu wote kwamba waonevu wamekanyaga kwa nguvu ardhi za Waislamu na hamu yao kubwa ya kutawala haishii Jerusalem peke yake, bali mpaka kwenye sehemu kubwa za ardhi za Kiislamu kama ilivyo dhahiri sasa kwa matukio katika Iraq na kufuatia unyanyasaji kwenye Jamhuri ya Kiislamu ya Iran .
Ni katika muktadha huu kwamba tunaadhimisha siku ya Quds. Ulimwenguni pote tunaadhimisha siku hii kwa maandamano na hutuba, tukijikumbusha sisi wenyewe, Ummah wa Kiislamu na kwa hakika ulimwengu wote kuhusu masaibu ya Masjid Al-Aqsa na ardhi ya Palestina. Masaibu ya Jerusalem na ya Palestina yenyewe ni alama ya masaibu ya nchi zote na mataifa yanayokandamizwa ulimwenguni pote, na kwa hakika, ukubwa mno wa alama hizo – zinaashiria uonevu wa nguvu za fahari za kidunia juu ya Nchi dhaifu – kwamba hakuna mahali popote katika ardhi ambako wanafanya kwa usahihi kabisa kuonyesha uovu na ushenzi wao kama katika ardhi ya Palestina.
Harakati za Wapalestina – hususan harakati zao za silaha – na uvamizi wa Al-Quds umeteka mawazo ya Waislamu. Ni kwa muda gani ulimwengu utaziba masikio yake ili usisikilize umwagaji damu wa Wapalestina mikononi mwa wavamizi? Je! Wapalestina hawapaswi kufurahia haki yao ya kuishi kwa uhuru katika ardhi yao kama watu wengine ulimwenguni? Uhalisi wa kimataifa ambao kwamba tulilinganiwa na ulimwengu kuutambua na kushikana nao unakanyagwa kila siku katika Palestina na jeshi la wavamizi na ongezeko lake la kijeshi na mazingira yanayowekwa katika miji yao, vijiji, kambi, na kusababisha umwagaji wa damu wa Wapalestina kwa mashine pofu za kijeshi zilizokusudiwa kwa ajili ya kuwaangamiza Waislamu na Masjid al-Aqsa.
Hivyo sehemu kubwa ya usikivu wakati inapokuja kwenye mshikamano wa Wapalestina ni katika Masjid al-Aqsa. Tangazo lilitolewa na Imam Khomeini la Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kama Yaum al-Quds (siku ya Quds) ni kumbu kumbu ya mwaka ya masaibu ya Wapalestina walionyang’anywa ardhi yao . Kwa Waislamu wote Masjidul Aqsa huko Al Quds (Jerusalem) inachukua sehemu muhimu sana baada ya Makka na Madina.
849515