IQNA

Ahmadinejad:

Utawala wa Kizayuni wa Israel hautadumu

21:41 - August 26, 2011
Habari ID: 2177079
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Mashariki ya Kati mpya imo katika hali ya kuumbika na masharti yake katika mizani ya watu wa eneo hili ni fikra za Kiislamu, heshima, izza na utukufu mwanadamu.
Ameongeza kuwa nchi za Magharibi na Wazayuni hawatakuwa na nafasi katika Mashariki ya Kati mpya.
Rais Ahmadinejad ambaye amehutubia maelfu ya waumini kabla ya Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa nguzo za utawala wa Israel zinalegalega na nchi za Magharibi zinajaribu kudhibiti hali hiyo kwa kuteka nyara matukio yanayojiri Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Ameashiria historia ndefe ya Palestina na kusema kuwa nchi za Magharibi zinahubiri mpango wa kuundwa nchi mbili za Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa shabaha ya kufunika jinai na uhalifu wao. Ameongeza kuwa kwa sasa Wapalestina wanamiliki asilimia 11 tu ya ardhi yao yote na kwamba kuwepo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel huko katika ardhi ya Palestina si tishio kwa Wapalestina pekee, bali kwa thamani zote za kibinadamu.
Rais Ahmadinejad amesema utawala wa kigadi wa Israel ndiyo nukta inayowakutanisha pamoja watenda jinai na wahalifu wote duniani na kwamba Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo imeadhimishwa leo kote duniani inawakutanisha pamoja watu wanaompwekesha Mwenyezi Mungu na kupinga dhulma kote duniani kwa ajili ya kufuta kabisa utawala huo dhalimu. 849965


captcha