IQNA

Kituo cha mazungumzo ya Uislamu na Ukristo chaanzishwa Ufilipino

14:42 - August 27, 2011
Habari ID: 2177320
Kituo cha Mazungumzo kati ya Uislamu na Ukristo kilifunguliwa pembeni ya msikiti mkuu wa Manila nchini Ufilipino hapo siku ya Alkhamisi ikiwa ni katika kunufaika na baraka za mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Shughuli za kituo hicho zitakuwa zikisimamiwa na Jumuiya ya Mazungumzo ya Kidini ya Silsila, ambayo itakuwa ikipanga ratiba, vikao na mazungumzo yote yatakayofanyika katika kituo hicho.
Waislamu na Wakristo wamefurahishwa mno na uzinduzi wa kituo hicho ambacho wanasema kitakuwa na nafasi muhimu katika kuandaa mazingira yanayofaa kwa ajili ya kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini mbili hizo muhimu za mbinguni.
Kituo hicho kitazinduliwa rasmi tarehe 20 Septemba ambapo viongozi wa Kiislamu na Kikristo na vilevile wa serikali na makundi ya kijamii na kisiasa wa Ufilipino wamealikwa kushiriki. 849937
captcha