IQNA

Nasrullah aonya kuhusu njama za Wazayuni za kuiyahudisha Quds

11:22 - August 28, 2011
Habari ID: 2177837
Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ametahadharisha kuhusiana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kubadilisha muundo wa kijamii wa Baytul Muqaddas huko Palestina na kuuyahudisha mji huo mtakatifu.
Akihutubia kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds iliyoadhimishwa kote ulimwenguni juzi, Nasrullah amesema bayana kwamba, Israel inataka kubadilisha muundo wa kijamii wa Baytul Muqaddas na kuuonyesha kwamba ni mji wa Mayahudi kupitia ujenzi usio halali wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ameitaka Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na viongozi wa ulimwengu wa Kiislamu kutambua rasmi haki ya Wapalestina ya kuwa na mji wa Baytul Maqaddas. Aidha ametaka kuundwa nchi huru ya Palestina ikijumuisha ardhi na maeneo yote ambayo ni mali ya Wapalestina. Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria hali ya mambo huko nchini Syria na kutahadharisha kuhusiana na uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.
850093
captcha