Sarah Leah Whitson mkuu wa watetezi wa haki za binadamu huko kaskazini mwa Afrika amesema, nyaraka zilizokusanywa hadi sasa zinaonyesha kuwa vikosi vya askari watiifu kwa utawala wa Gaddafi viliwaua raia wengi wakati wanamapinduzi walipoingia mjini Tripoli. Ripoti hiyo imeongeza kuwa viwiliwili vya watu 18 wakiwemo wawili ambao mikono yao ilikuwa imefungwa, vimegunduliwa katika kizuizi cha mto mmoja karibu na eneo la ngome ya Muammar Gaddafi ya Babul Aziziya.
Watu walioshuhudia wamewaeleza watetezi hao wa haki za binadamu kuwa watu hao waliuawa na vikosi vya askari wa Gaddafi.850836