Mkuu wa Idara hiyo Dr. Mohammad Hadi Ayazi amesema kuwa mji wa Tehran una mipango mingi tajiri ya Qur'ani Tukufu ambayo inapaswa kuakisiwa kimataifa.
Amesema Baraza Kuu la Qur'ani limebuniwa na Manispaa ya Tehran. 'Mwenyekiti wa Baraza hili ni Meya wa Tehran na kati ya majukumu yake ni kuratibu harakati za Qur'ani katika mji huu na kuandaa sera za kustawisha harakati hizo".
Amesema, katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka jana na mwaka huu, hema za Qur'ani zimewekwa katika mitaa mbalimbali hatua ambayo imepongezwa na wakazi wa Tehran.
851082