Hujjatul Islam Hamid Mohammadi , Mkuu wa Kituo cha Uratibu na Ustawi wa Shughuli za Qur’ani katika Baraza la Mji wa Tehran amemwabia mwandishi wa IQNA kuwa mpango huo utatekelezwa kutokana na juhudi za baraza hilo pamoja na baraza la mji.
Ameongeza kuwa taasisi nyinginezo ikiwa ni pamoja na vyuo vya kidini na vituo vya Qur’ani vinashirikiana katika mpango huo.
Hujjatul Islam Mohammadi amesema mpango huo unalenga kukidhi mahitaji ya jamii na kustawisha utamaduni wa Qur’ani. Amesema kuwa mpango huo tayari umeshaanza katika baadhi ya mabustani ya Tehran.
Mji wa Tehran wenye wakazi zaidi ya milioni 12 una maelfu ya mabustani ambayo yameenea katika mitaa yote.
852558