IQNA

Hamas yaipongeza Uturuki kwa kumfukuza balozi wa Israel

11:55 - September 03, 2011
Habari ID: 2180335
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imeipongeza Uturuki kutokana na hatua yake ya kumfukuza nchini humo balozi wa utawala haramu wa Israel.
Ikitoa taarifa hapo jana Ijumaa harakati hiyo ya Kiislamu imeisifu hatua ya serikali ya Ankara ya kupunguza uhusiano wake wa kisiasa na utawala huo na kumfukuza balozi wake kutoka mjini humo. Imesema hatua hiyo ni nzuri na ya kupongezwa katika kujibu shambulio la kijeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya msafara wa meli za misaada kwa Wapalestina wa Uhuru ambapo wanaharakati kadhaa wa haki za binadamu na wafikishaji misaada wa Uturuki waliuawa. Hamas imetangaza kufurahishwa kwake na hatua hiyo ya serikali ya Uturuki na kuomboleza na familia za wahanga wa tukio hilo la mauaji. Imesema inaunga mkono kikamilifi juhudi za serikali ya Ankara za kuufikisha utawala huo kwenye mahakama ya kimataifa kuhusiana na mauaji hayo.
Hamas imezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kususia bidhaa za utawala haramu wa Israel na kufanya juhudi za kuvunja mzingiro unaotekelezwa na utawala huo dhidi ya Ukanda wa Gaza na vilevile kuunga mkono juhudi za kuundwa taifa huru la Palestina.
Harakati nyingine ya Kiislamu ya Palestina Jihadul Islami pia imeipongeza Uturuki kwa hatua yake ya kumfukuza balozi wa Israel. 853446
captcha