IQNA

Duru ya pili ya kimataifa ya mafunzo ya majaji wa Qur'ani Saudia

15:35 - September 03, 2011
Habari ID: 2180552
Duru ya pili ya kimataifa ya mafunzo ya majaji wa Qur'ani Tukufu itafanyika katika mji mtakatifu wa Makka pambizoni mwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu.
Mafunzo hayo ya majaji wa Qur'ani yatasimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia tarehe 19-26 Disemba.
Katika kipindi hicho cha wiki moja, washiriki kutoka nchi mbalimbali watapewa mafunzo ya kanuni za ujaji katika hifdhi ya Qur'ani, kutayarisha majaji kwa ajili ya mashindano ya Qur'ani na kulea majaji kwa ajili ya viwango vya kimataifa.
Miongoni mwa masharti ya washiriki katika mafunzo hayo ni kuwa na umri wa juu ya miaka 20 na chini ya miaka 45, kuhifadhi Qur'ani nzima na kuwa ya tajiriba katika masuala ya kielimu na kutoa mafunzo. 853633


captcha