IQNA

Gaddafi anajitayarisha kukimbilia Nigeria

15:34 - September 03, 2011
Habari ID: 2180554
Msemaji wa wanamapinduzi wa Libya amesema kuwa dikteta wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi anajitayarisha kwa ajili ya kukimbilia nchini Nigeria.
Ahmad Bani anasema kuwa ujumbe uliotolewa hivi karibuni na Gaddafi unaonyesha kuwa dikteta huyo amechukua uamuzi wa kukimbilia nje ya nchi.
Ameeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa Gaddafi akakimbilia Nigeria na kuongeza kuwa ripoti zinasema kuwa dikteta huyo yuko katika mji wa Sabha ulioko kusini mwa Libya.
Msemaji wa kijeshi wa wanamapinduzi wa Libya amesema kuwa umetolewa muhula wa wiki moja wa kuwataka wapiganaji wa Gaddafi wajisalimishe katika mji wa Sirte ili kulinda maisha ya raia.
Amesema kuwa mji huo unadhibitiwa na watenda jinai wanaoogopa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.853397


captcha