Waislamu wa Nairobi wamesimamisha Sala ya Idi katika uwanja wa Sir Ali na maeneo mengine mjini humo.
Huko Mombasa Waislamu walisali Sala ya Idi katika karibu misikiti yote na vilevile katika viwanja vya Tononoka na Shule ya Msingi ya Ziwani chini ya ufadhili wa Wqfu wa Sharif Nassir.
Katibu Mwandalizi wa SUPKEM Sheikh Shariff Hussein amesema baraza hilo litaitisha mkutano wa kitaifa wa viongozi wa Kiislamu wa Kenya kujadili njia za kutatua tofauti zilizopo kuhusu suala la mwezi mwandamo hasa kuhusu kuanza na kumalizika mwezi wa Ramadhani. Amesema aghalabu ya Waislamu Kenya waliswali Sala ya Idul Fitr Jumatano kufuatia tangazo rasmi la Kadhi Mkuu Sheikh Ahmad Shariff Hussein Muhdhar. Baadhi ya Waislamu wa Kenya waliswali Sala ya Idi Jumanne iliyopita.
853821