Katika mazungumzo ya simu na Khalid Meshaal mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas Rais Ahmadinejad amempongeza kiongozi huyo wa Hamas, wanamapambano na taifa la Palestina kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Fitr. Amesema ana matumaini kuwa Mwenyezi Mungu SW amewatakabalia Wapalestina dua ya uhuru katika nyusiku za Laylatul Qadr. Rais Ahmadinejad amesema Iran itaendelea kuwa pamoja na wanamapambano na taifa la Palestina hadi watakapofikia malengo yao na kupata uhuru.
Naye Khalid Meshaal amempongeza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais na taifa la Iran kwa mnasaba wa Idul Fitr. Amesema taifa la Palestina litaendeleza mapambano hadi ushindi upatikane.
Meshaal amesema wanamapambano na taifa la Palestina linaishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuendelea kuunga mkono harakati za kupigania uhuru za Palestina. 854005