IQNA

Jamii ya kimataifa yakosolewa kwa kuzembea kuhusu kadhia ya Imam Musa Sadr

11:41 - September 04, 2011
Habari ID: 2180908
Hassan Ya'qub, mwanaye Sheikh Muhammad Ya'qub, aliyetekwa nyara pamoja na Imam Musa Sadr nchini Libya ameikosoa jamaii na mashirika ya kimataifa kwa kuzembea katika kufuatilia kadhia ya Imam Musa Sadr na wenzake wawili.
Amesisitiza kwamba utekaji nyara huo ni suala la kitaifa na kibinadamu ambalo linapswa kupewa umuhimu mkubwa na kufuatiliwa kwa karibu.
Akizungumza hivi karibuni kwa mnasaba wa kuwadia miaka 33 tokea mwanazuoni huyo wa Kiislamu atekwe nyara, Hassan Ya'qub amesema kuwa taifa la Lebanon halitachoka kufuatilia kadhia hiyo kwa sababu inaimarisha umoja na mshikamano wa wananchi wa nchi hiyo. Ameongeza kuwa jambo hilo linapewa umuhimu mkubwa na Walebanon wote bila kujali kabila, dini na madhehebu yao. Ameshangazwa na uzembe pamoja na upuuzaji unaofanywa na jamii ya kimataifa kuhusiana na suala la kutekwa nyara Imam Musa Sadr, ilihali Kurt Joseph Waldheim, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa alitangaza kwamba utekaji nyara wa Imam Sadr lilikuwa suala muhimu la karne ya 20. Licha ya tangazo hilo muhimu, lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa na taasisi wala mahakama za kimataifa kufuatilia jambo hilo.
Hassan Ya'qub amewabashiria wapenzi na wafauasi wa Imam Musa Sadr na wenzake wawili habari njema kwamba mateka hao wangali hai na kwamba hivi karibuni wataachiliwa huru na kurejea katika nyanja mbalimbali za kisiasa na kijamii. 853760
captcha