IQNA

'Mwamko wa Kiislamu hii leo umeathiri ulimwengu'

12:37 - September 05, 2011
Habari ID: 2181469
Dakta Ali Akbar Velayati, Katibu Mkuu wa mkutano wa kwanza wa mwamko wa Kiislamu amesema kuwa, hii leo ulimwengu umeathirika na mwamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu.
Amesema, Wamagharibi wanafanya njama za kuzuia kuzaa matunda kwa mwamko wa Kiislamu hivyo kuna haja ya Waislamu kuwa macho zaidi. Ali Akbar Velayati ambaye pia ni Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa ameashiria nyendo za Marekani na Shirika la Kijeshi la NATO katika nchi za Kiislamu na kubainisha kwamba, baadhi ya nchi za Magharibi zimejikita katika matukio ya ulimwengu wa Kiislamu.
Katibu Mkuu wa mkutano wa kwanza wa mwamko wa Kiislamu ameashiria pia ushindi wa mapinduzi ya Libya na akasema kuwa, wananchi wa Libya wamefanikiwa kumuangusha Kanali Muammar Gaddafi kwa hima yao.
Mkutano wa kwanza wa mwamko wa Kiislamu utafanyika tarehe 17 na 18 za mwezi huu wa Septemba hapa mjini Tehran na unatarajiwa kuhudhuriwa na wanafikra 700 kutoka nchi 80 duniani.
854291
captcha