IQNA

Maonyesho ya Picha za Mwamko wa Kiislamu kufanyika Tehran

12:39 - September 05, 2011
Habari ID: 2181483
Mkuu wa Jumuiya ya Wapiga Picha Iran amesema Maonyesho ya Picha za Mwamko wa Kiislamu duniani yatafanyika mjini Tehran.
Rasul Oliyazadeh amesema maonyesho hayo yatajumuisha picha 200 zilizochukuliwa katika mwamko wa Kiislamu huko Libya, Misri,Tunisia, Bahrain na Yemen.
Amesema picha hizo zimechaguliwa kutoka picha zilizotumwa na wapiga picha wa nchi hizo na zitaonyeshwa kwa muundo wa posti kadi.
Amesema kuwa picha hizo za mwamko wa Kiislamu pia zitasambazwa katika idara mbalimbali za serikali kote Iran. Amesema picha bado zinaendelea kupokelewa kutoka maeneo mbalimbali duniani.
853661
captcha