IQNA

Mazungumzo ya simu ya Ayatullah Sistani na Ayatullah Isa Qasim wa Bahrain

12:43 - September 05, 2011
Habari ID: 2181518
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani wa Iraq amezungumza kwa njia ya simu na mwanazuoni mwenzake Ayatullah Sheikh Isa Qasiim wa Bahrain kwa lengo la kujadili hali ya Waislamu wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya al-Bayan, Ayatullah Sistani amemjulia hali ya kiafya Sheikh Qassim pamoja na Waislamu wa Bahrain wanaoendelea kukandamizwa na utawala wa Aal Khalifa kwa ushirikiano wa Aal Saud wa Saudia Arabia.
Ayatullah Sistani amemwombea dua mwenzake huyo na Waislamu wa nchi hiyo kwa ujumla na kumhakikishia kwamba anafanya kila awezalo ili kutatua matatizo ya umma wa Kiislamu na hasa ya Waislamu wa Bahrain.
Kwa upande wake Ayatullah Isa Qassim amemshukuru Ayatullah Sistani kwa mawasiliano hayo ya simu na juhudi anazofanya kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano katika umma wa Kiislamu. 854195
captcha