Binti Mfalme huyo ambaye ni mpwa wa Mfalme Abdullah na mwanaharakati wa kijamii amesema asilimia 95 ya Wasaudi wanaishi chini ya mstari wa umasikini ulioainishwa nchini humo. Amesema Wasaudi wengi hawana suhula za kimsingi kama vile maji na umeme. Hii ni katika hali ambayo asilimia tano ya Wasaudi ndio wanaofaidika na utajiri mkubwa wa nchi hiyo.
Aidha amefichua kuwa watawala wa Saudi Arabia walipora dola (US$) bilioni 21 ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kupanua Msikiti Mtakatifu wa Makka.
Mwanaharakati wa kijamii na kisiasa Saudi Arabia Mohammad al-Qahtarni amethibitisha tuhuma hizo na kusema familia ya Aal Saudi inamiliki nguvu na utajiri wote wa Saudi Arabia.