Kwa mujibu watovuti ya Atlasinfo, walowezi hao wa Kiyahudi walichoma moto msikiti wa Dhu Nurein na kuharibu suhula zake nyingi.
Taarifa hiyo inasema kuwa kuna haja ya kuchukuliwa hatua kali zaidi za usalama ili kuzuia kukaririwa kwa kitendo kama hicho cha jinai. Imesema kuwa kushambuliwa na kuharibiwa maeneo ya ibada ya Waislamu ni dhahirisho halisi la ukiukaji wa uhuru na haki za kiraia za Waislamu.
Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC amesema katika taarifa hiyo kwamba viongozi wa utawala haramu wa Israel ndio wahusika wakuu wa vitendo hivyo vinavyotekelezwa mara kwa mara na walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, mali na maeneo yao ya ibada. Amezitaka taasisi za kimataifa kuchukua hatua za dharura ili kusimamisha mara moja vitendo hivyo vya jinai vya Wazayuni kwa sababu vinaweza kuvuruga zaidi hali ya utulivu wa ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakishambulia na kuchoma moto misikiti ya Waislamu wa Palestina ambapo hivi karibuni waliteketeza pia Msikiti wa al-Anbiyaa katika nojawapo ya vijiji vya Beit al-Laham. 855419