Huku akidai kwamba watu aliowataja kuwa ni makundi ya mifarakano hawawezi kugundua sehemu aliko dikteta huyo, Ibrahim amesema kuwa Gaddafi angali yuko nchini Libya na kwamba maadui wake hawatampata. Amesema utawala wake ungali una nguvu nchini humo na kwamba wanawe ndio wanaoendesha masuala ya nchi na kuchukua hatua zote muhimu za kuilinda nchi hiyo.
Musa Ibrahim ameongeza kuwa wanawe hao wako tayari kufa kwa ajili ya kuilinda nchi yao.
Amesema kuwa Seiful Islam mwanawe Gaddafi pia angali yuko nchini humo. Amesisitiza kwamba kamwe Libya haitaanguka mikononi mwa wanamapinduzi na kwamba makabila ya nchi hiyo yanafanya kila liwezekanalo ili kuilinda na kwamba wataendeleza mapambano yao hadi watakapokomboa miji yote iliyotekwa na wanamapinduzi. 855440