Nyaraka hizo za siri ziliratibiwa tarehe 24 Januari mwaka 2007. Kwa mujibu wa nyaraka hizo Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilimtaka Mubarak aikabidhi nyaraka na maelezo ya siri kuhusiana na vituo vya nyuklia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Nyaraka hizo zilitayarishwa na Husam Ali, mkuu wa Idara ya Misri ya Upokonyaji Silaha katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, baada ya kuvitembelea vituo vya nyuklia vya Iran.
Nyaraka hizo za Wikileaks zinaonyesha kwamba maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani walionana na Husam Ali kabla ya kufanya safari yake nchini Iran na kumjulisha mambo waliyotaka ayafuatilie katika safari yake hiyo ya kuvikagua vituo vya nyuklia vya Iran. 855104