Hizbullah imesema kuwa ripoti hiyo na Umoja wa Mataifa inahalalisha mzingiro wa Wazayuni dhidi ya raia wasiokuwa na ulinzi wa Ukanda wa Gaza.
Taarifa ya Hizbullah imesema katika ripoti yake kwamba ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inatia aibu na inataka kuhalalisha mzingiro wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wa Gaza.
Wanaharakati 9 wa kutetea haki za binadamu waliuawa katika shambulizi lililofanywa na askari wa Israel miezi kadhaa iliyopita dhidi ya meli iliyokuwa na misaada ya kibinadamu kwa ajili ya raia wanaozingirwa wa Gaza.
Hizbullah imesema kuwa ilitazamiwa kwamba Umoja wa Mataifa utachukua hatua kama hiyo kwani huko nyuma pia umekuwa ikihalalisha jinai na uhalifu wa utawala huo dhalimu.
Hizbullah imesisitiza kuwa nchi mbalimbali zinapaswa kuelewa kuwa zinapaswa kushughulikia matatizo yao zenyewe bila ya kutegemea jumuiya za kimataifa ambazo zimekuwa ukumbi wa viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 855593