IQNA

‘Mazungumzo ya Kidini’, njia muafaka ya mazungumzo ya Uislamu na Magharibi

15:45 - September 07, 2011
Habari ID: 2182859
Mahmud Hamdi Zaqzouq mwandishi wa kitabu ‘Uislamu na Magharibi’ anaamini kuwa njia bora zaidi ya mazungumzo muafaka kati ya Uislamu na Magharibi ni kupitia mazungmzo ya kidini.
Haya ni kwa mujibu wa mwanazuoni wa historia na mtafiti Bi. Mansoureh Parvini.
Akizungumza Septemba nne katika kikao cha kujadili kitabu hicho, amesema makabiliano, mawasiliano ya upande moja, vitisho na tuhuma ni mambo ambayo hayawezi kusaidia mazungumzo ya Uislamu na Magharibi.
Amesema mwandishi wa kitabu hicho hafurahishwi na ufa uliopo baina ya jamii za umma wa Kiislamu na Magharibi. Amesema ufa huo unazidi kupanuka na hivyo anaona haja ya kuchapisha kitabu hicho ili kuwasaidia watafiti na kuwasilisha mapendekezo yake.
Bi Parvini amesema nguvu ya kitabu hicho ni ukosoaji wake wa mustashriqin (Orientalists) na wataalamu wa Uislamu katika nchi za Magharibi. Anasema Zaqzouq pia anawakosoa Waislamu kwa kutochukua hatua zinazofaa kukabiliana na upotoshaji wa Uislamu katika nchi za Magharibi.
854742
captcha