Sheikh wa al- Azhar amehoji ni vipi sheria za kimataifa zinaweza kuruhusu kufanyika hujuma ya kinyama dhidi ya msafara wa meli za misaada ya kibinadamu kwa wahitaji kama ile hujuma iliyofanywa na makomandoo wa utawala wa Israel dhidi ya msafara wa Uhuru uliokuwa ukiwapelekea misaada ya kibinadamu wakazi wa Ukanda wa Gaza tena katika maji ya kimataifa?
Sheikh Tayyib amesema mashambulo ya kinyama yanayofanywa mara kwa mara na askari wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya misafara kama hiyo ya misaada ya kibinadamu si jambo geni na kwamba walimwengu wanalifahamu vyema.
Sheikh Ahmad Tayyib ameshangazwa na uungaji mkono wa Ban Ki-Moon kwa ripoti ya upendeleo ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa iliyotayarishwa na Geoffrey Palmer kuhusiana na Gaza na kuongeza kuwa madhalimu na watu wanaounga mkono ripoti hiyo watajuta kesho.
Ripoti hiyo imewashangaza wengi duniani kwa kuunga mkono mzingiro wa kidhulma unaotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kupuuza takwa la Uturuki la kuutaka uiombe msamaha kwa kushambulia Msafara wa Uhuru kwenye maji ya kimataifa na kuwaua raia wake 9. 855913