IQNA

Wasomali 750,000 kuaga dunia katika miezi minne ijayo

15:42 - September 07, 2011
Habari ID: 2182958
Umoja wa mataifa umeonya kwamba huenda Wasomali 750,000 wakaaga dunia katika kipindi cha miezi minne ijayo iwapo misaada ya dharura ya kibinadamu haitawafikia kwa wakati.
Kwa mujibu wa gazeti la Independent la Uingereza, maeneo sita kusini mwa Somalia yanakabiliwa na janga kubwa la njaa na kwamba yanahitaji misaada ya dharura ili kuokoa maisha ya wahitaji katika maeneo hayo.
Zaidi ya nusu ya watu milioni 4 wa nchi hiyo wanahitaji misaada ya dharura ya chakula, na bila shaka makumi ya watu katika nchi jirani za Kenya, Ethiopia, Djibouti na Uganda ambazo pia zinakabiliwa na tatizo la ukame katika baadhi ya sehemu za nchi hizo, pia huenda wakapoteza maisha iwapo hawatashughulikiwa haraka.
Kufikia sasa watu wapatao 150,000 wameshakimbia nyumba zao na kutafuta misaada ya chakula kwenye kambi za wakimbizi nchini Somalia.
Misaada mingi ya chakula imeshapelekwa nchini humo lakini kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa misaada hiyo bado haitoshi kukidhi mahitaji ya watu wengi wanaokabiliwa na baa la njaa katika pembe tofauti za nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. 855910
captcha