Tovuti hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi hapo jana Jumanne inatoa fursa hiyo kwa Waislamu wote duniani.
Kwa mujibu wa mpango huo, kila Mwislamu ambaye ana hamu ya kuzuru makaburi hayo matukufu lakini hana nafasi ya kufanya hivyo mwenyewe moja kwa moja kutokana na sababu moja au nyingine, anaweza kujiandikisha kwenye tovuti hiyo kwa lugha ya Kiarabu na kufanyiwa ziara hiyo kwa niaba, yaani kupitia mtu mwingine.
Mpango huo ambao umekaribishwa na Waislamu wengi unamtaka mtu aliye na nia ya kuyazuru makaburi ya watukufu hao kwa niaba au wakala kuandikisha jina, anwani ya barua pepe na nchi yake katika sehemu maalumu kwenye tovuti hiyo ili apate fursa ya kufanyiwa ziara hiyo na mtu aliye mjini Madina bila malipo yoyote.
Makaburi ya Baqii au kwa jina jingine Jannat al-Baqii yanajumuisha makaburi ya maimamu wanne wa madhehebu ya Shia ambao ni Maimamu Hassan, Sajjad, Muhammad Baqir na Jaafar Swadiq (as). Vilevile wengi wa wake wa Mtume (saw), Abbas ami yake Mtume (saw) Fatima bint Asad ambaye ni mama yake Imam Ali bin Abi Twalib (as) na watukufu wengine wengi wa Kiislamu wamezikwa katika makaburi hayo ambayo yako pembeni ya Msikiti wa Mtume (saw) mjini Madina.
Walio na hamu ya kusajili majina yao wanaweza kufanya hivyo kupitia anwani ifuatayo: http://alkafeel.net/albaqee/zyara/
855924