Kwa mujibu wa gazeti linalochapioshwa Kenya la Business Daily Africa, eneo lenye Waislamu wengi la Eastleigh mjini Nairobi lina hospitali, kliniki na duka za dawa zinazotoa huduma za tiba halali.
Katika hospitali au kliniki zinazotoa huduma halali, suala la vyakula na dawa linazingatiwa ili kuhakikisha kuwa misingi ya Kiislamu inafuatwa. Aidha vituo hivyo vya afya vimetenga vyumba maalumu kwa ajili ya Waislamu kusalia.
Hivi sasa kuna mpango wa kujenga hospitali mpya katika eneo hilo ambayo usanifu majengo wake utazingatia masuala mbalimbali ya Kiislamu.
856677