Fatuwa ya kuvunjwa makaburi hayo ya watoto na wajukuu wa Mtume Muhammad SAW ilitolewa na Kadhi Mkuu wa Kiwahabi Sheikh Abdullah bin Baliid baada ya Muhammad bin Saud kudhibiti maeneo mengi ya Hijaz ukiwemo mji mtukufu wa Madina.
Mawahabi hao waliwakusanya wananchi kwa nguvu ya silaha na kuwalazimisha kuvunja jengo lililokuwa na makaburi ya Ahlul Bait wa Mtume SAW katika eneo la Baqii. Jengo hilo lilikuwa na makaburi ya wajukuuu wanne wa Mtume, mtoto wa mtukufu huyo Ibrahim SA na kadhalika. Jengo pekee lililonusurika na mashambulizi hayo ya kinyama ya Mawahabi ni lile lililokuwa na kaburi tukufu la Bwana Mtume SAW ambalo Mawahabi hao waliogopa kulivunja kwa kuhofia hasira kubwa za Waislamu.
Siku hiyo ya kusikitisha imesajiliwa katika historia ya Kiislamu kwa jina la"Yaumul Hadm"kwa maana ya siku ya vunjavunja.
856555