IQNA

Maujai yachochewa dhidi ya Waislamu kwenye Facebook

17:46 - September 10, 2011
Habari ID: 2184217
Baadhi ya watu nchini Ufaransa wameanzisha ukurasa maalumu katika mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo wanawachochea wasomaji wa ukurasa huo wafanye mauaji dhidi ya Waislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya lepoint ukurasa huo ambao ulianzishwa siku ya Jumatano kwa jina la 'Waueni Waisamu katika Idi yao ya Adh'ha' unawataka watu walio na chuki na uadui dhidi ya Uislamu wawachinje Waislamu katika siku ya kuadhimishwa sikukuu hiyo muhimu katika kalenda ya Kiislamu.
Jumuiya ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu ya Ufaransa CCIF imeitaka Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na kituo cha polisi katika Idara ya Mahakama ya Ufaransa kuchukua hatua za dharura ili kutambua na kuwatia mbaroni wahusika wa kitendo hicho cha uchochezi na jinai dhidi ya Waislamu.
Vilevile wakuu wa mtandao wa Facebook wametakiwa kufuta ukurasa huo mara moja ili kuepusha jinai inayoweza kufanyika dhidi ya Waislamu katika siku ya Idul Adh'ha.
Jambo la kusikitisha ni kwamba ombi la jumuiya hiyo bado halijajibiwa na polisi ya Ufaransa wala wakuu wa mtandao wa Facebook. 857257
captcha