Gavana huyo ametoa amri ya kufutiliwa mbali maandamano hayo baada ya awali kutolewa kubali cha kufanyika maandamano hayo dhidi ya Uislamu.
Katika taarifa yake gavana wa mji huo amesema kuwa amechukua uamuzi wa kufutilia mbali maandamano hayo baada ya kutambua kuwa yanaweza kuchochea chuki za kijamii na vurugu katika mji huo.
Ijumaa ya jana baadhi ya maseneta wa Ufaransa walimtumia barua Jean Claud, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa wakimtaka afutilie mbali maandamano hayo kutokana na uwezekano wa kuchochea hisia za chuki, ghasia na ubaguzi dhidi ya jamii ya Waislamu wa nchi hiyo.
Waislamu wa mji wa Forbach awali walikuwa wametangaza kuwa wangefanya maandamano yao sambamba na maandamano hayo ili kulalamikia ongezeko la chuki na ubaguzi dhidi yao. 857550