IQNA

Wanamapinduzi Libya waingia mjini Ban Walid

18:00 - September 10, 2011
Habari ID: 2184381
Wanamapinduzi wa Libya wameanza kupambana na vikosi vitiifu kwa Muammar Gaddafi kwenye mji wa Bani Walid baada ya kuuzingira mji huo kwa zaidi ya wiki moja.
Taarifa zinasema kuwa wapiganaji 23 wanaomuunga mkono Gaddafi wameuawa katika mapigano hayo na wengine 9 kutiwa mbaroni.
Wanamapinduzi ambao tayari wameulazimisha utawala wa Gaddafi kuondoka katika mji mkuu Tripoli, wameingia katika mji wa Bani Walid baada ya mazungumzo ya pande mbili ya kuepusha umwagaji damu kushindwa kuzaa matunda.
Mji huo wa kistratejia ni moja ya miji ambayo bado inadhibitiwa na wafuasi wa Gaddafi. Miji mingine ni Jufrah, Sabha na Sirte alikozaliwa Gaddafi. 857755
captcha